Umoja wa Madaktari Nchini #Uganda (UMA) umepinga suala la kulazimisha watumishi wa Afya na Raia kupatiwa chanjo ya #COVID19 kilazima. Wametahadharisha kuwa yatakapotokea matokeo yoyote Serikali itawajibika
Uganda imepata upinzani hata kwa Wahudumu wa Afya ambao hawajawa tayari kuchoma Chanjo. Rais wa UMA, Dkt. Richard Idro amesema Afya ya mtu ni suala binafsi haina haja ya kulazimisha
Kauli hiyo imekuja kufuatia Viongozi kadhaa wa Kisiasa kwenye baadhi ya Wilaya kutaka Watumishi wa Afya wapatiwe Chanjo kilazima. Wametolea mfano Wilaya ya Amuru walipokea Chanjo 3,000 ambapo waliochoma ni 45 tu
Wizara ya Afya imeripoti kuwa tangu Aprili 13 hadi sasa ni Watumishi wa Afya 20,405 kati ya takribani 150,000 ndio wamechoma Chanjo. UMA wameshauri kampeni za kujenga uelewa wa Chanjo zifanyike