Umoja wa Mataifa wamkumbuka Magufuli kwa aliyoifanyia Tanzania




 



Baadhi ya viongozi katika kikao cha 75 cha mkutano wa 59 wa Umoja wa Mataifa (UN) uliofanyika leo Ijumaa Aprili 16, 2021 wamebainisha alama za uongozi za rais wa awamu ya tano wa Tanzania, Hayati John Magufuli wakishauri kuendelezwa na kuahidi kushirikiana na Rais Samia Suluhu Hassan.


Kikao hicho kilichoongozwa na Volkan Bozkir ambaye ni Rais wa baraza kuu la UN kilikuwa na ajenda mbalimbali  ikiwemo ya kutambua mchango wa Magufuli aliyefariki dunia kwa ugonjwa wa moyo Machi 17, 2021 mkoani Dar es Salaam.



Akitaja baadhi ya maeneo ya kumuenzi Magufuli, katibu mkuu wa umoja huyo, António Guterres amesema atakumbukwa kwa mchango wake katika kurejesha maadili ya utumishi wa umma, kupambana na rushwa, ujenzi wa miundombinu na mapinduzi ya viwanda ambayo ni msingi katika ukuaji uchumi.



“Tanzania imefanikiwa kufikia nchi ya watu wenye kipato cha kati miaka minne kabla ya kufikia 2025, alifanikiwa kuwezesha mfumo wa elimu bila malipo iliyowezesha watoto wengi kuongezeka shuleni, pia alifanikiwa kusogeza huduma za umeme vijijini kwa jitihada za kufikia wananchi wengi.”



“kwa niaba ya umoja wa mataifa ninatoa pole kwa familia, natumia nafasi hii kuahidi umoja wa mataifa kuendelea kufanya kazi kwa ukaribu na Serikali iliyopo chini ya Samia Suluhu Hassan, tuko pamoja na raia wa Tanzania katika juhudi zao za kujiletea maendeleo,” amesema Guterrez.



 Mwakilishi kutoka Ulaya Magharibi, amesema rais Magufuli alikuwa kiongozi aliyejitoa kwa ajili ya kuwaletea Watanzania maendeleo na kwamba juhudi zake zilitambulika kwa kiwango kikubwa kupitia sekta ya elimu na miundombinu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad