Utafiti: Watu weusi wanachukiwa zaidi Marekani wanaongoza kuuawa na polisi, hizi sababu tatu

 
Tumefanya utafiti wa takwimu za rangi na matabaka ya kijamii na ambavyo wanaathirika na mfumo wa utoaji haki na kuzuia uhalifu nchini Marekani.



1. Wamarekani Weusi wako hatarini zaidi kuuawa na polisi

Takwimu ambazo zipo wazi kwa matukio ambayo polisi wameua raia kwa risasi zinaonesha kuwa kwa Wamarekani Weusi kuna uwezekano mkubwa zaidi wa kupigwa risasi na kuuawa ukilinganisha na idadi yao kwa ujumla nchini humo.

1. Wamarekani Weusi wako hatarini zaidi kuuawa na polisi
Takwimu ambazo zipo wazi kwa matukio ambayo polisi wameua raia kwa risasi zinaonesha kuwa kwa Wamarekani Weusi kuna uwezekano mkubwa zaidi wa kupigwa risasi na kuuawa ukilinganisha na idadi yao kwa ujumla nchini humo.

Fatal shootings chart
Kwa mujibu wa kanzidata ya gazeti la Washington Post jus ya matukio ya polisi kupiga watu risasi, japo Wamarekani wenye asili ya Africa ni chini ya asilimia 14 ya raia wote wa Marekani, lakini wao ni wahanga kwa asilimia 24 ya matukio 6,000 ya polisi kuuwa watu kwa risasi toka mwaka 2015.

Idadi ya vifo vinavyotokana na kupigwa risasi na polisi nchini Marekani imeendelea kusalia kuwa takriban watu 1,000 kwa mwaka toka 2015.

Takwimu pia zinaonesha kuwa uwiano wa polisi kuwashambulia kwa risasi watu weusi ambao hawajajihami kwa silaha ni mkubwa mara tatu zaidi ya wazungu.

2. Uwezekano wa kusimamishwa barararani ni mkubwa zaidi

Tafiti zinaonesha kuwa watu weusi wapo kwenye uwezekano mkubwa zaidi wa kusimamishwa na askari wa barabarani nchini humo.

Protestor holding a placard with picture of George Floyd
Utafiti wa hivi karibuni zaidi ni wa mwaka 2020 uliofanywa na Chuo Kikuu cha Stanford na kupitia matukio milioni 100 ya watu kusimamishwa barabarani kote nchini Marekani. Matokeo yake yakawa ni madereva weusi wapo kwenye uwezekano wa kusimamishwa kwa zaidi ya asilimia 20 ukilinganisha na wazungu.

Na hata baada ya kusimamishwa, utafiti huo umebainisha kuwa madereva weusi walipekuliwa mara mbili zaidi ya madereva wazungu, japo madereva weusi kitakwimu uwezekano wa kuwa wamejihami kwa silaha haramu ni mdogo zaidi.

3. Wamarekani weusi wanakamatwa zaidi kwa matumizi ya mihadarati
Wamarekani wenye asili ya Afrika wanakamatwa zaidi kwa matumizi ya mihadarati kuliko wazungu japo tafiti zinaonesha kuwa matumizi ya mihadarati inawiana kwa jamii hizo mbili.

Mwaka 2018, takriban watu 750 kati ya kila wamarekani weusi 100,000 walikamatwa kea matumizi ya mihadarati, ukilinganisha na yatu 300 kati ya wazungu 100,000.

Black man under arrest with hands on head
Tafiti za nyuma za matumizi ya mihadarati nchini humo zinabainisha kuwa wazungu hutumia mihadarati kwa kiwango sawa na weusi, japo watu weusi hukamatwa zaidi.

Mathalan utafiti uliofanywa na taasisi ya American Civil Liberties Union uligundua kuwa wamarekani weusi wanaweza kukamatwa kwa kuwa na bangi mara 3.7 zaidi ya wazungu japo matumizi ya bangi baina ya jamii hizo mbili yanawiana.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad