Vanessa Bryant amekanusha taarifa zilizotoka kwamba familia ya Kobe Bryant imekataa Ku-renew mkataba na kampuni ya NIKE



Vanessa Bryant amekanusha taarifa zilizotoka kwamba familia ya Kobe Bryant imekataa Ku-renew mkataba na kampuni ya NIKE ambayo ilikuwa ikishirikiana na Kobe kutengeneza bidhaa za viatu.


Kupitia ukurasa wake wa instagram, Vanessa ambaye ni mjane wa Kobe Bryant amesema mkataba huo uliisha muda wake (expire) April 13, 2021 na ameapa kupambana kurudisha ushirikiano na Nike kwa ajili ya mashabiki na wanamichezo ambao walizipenda bidhaa za Kobe.

-

"Mkataba wa Kobe uliisha muda wake April 13, 2021. Kobe na Nike walitengeneza kati ya viatu bora na vizuri vya Kikapu kwa muda wote, vikivaliwa na kuhusudiwa na mashabiki pia wanamichezo kwenye michezo yote kote duniani.

-

"Tumaini langu siku zote litakuwa kuruhusu mashabiki wa Kobe kupata na kuvaa bidhaa zake. Nitaendelea kupambana kwa ajili ya hilo. Bidhaa za Kobe zinauza ndani ya sekunde. Hilo linajieleza wazi. Nilikuwa natumai kutengeneza ushirikiano wa muda mrefu na Nike ambao unalandana na heshima aliyoiacha mume wangu. Siku zote tutafanya kila liwezekanalo kuwaenzi Kobe na Gigi. Hili halitobadilika." aliandika Vanessa Bryant kwenye insta stories.

6h

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad