Viatu ambavyo mtindo wake ulibuniwa na kuvaliwa na mwanamuziki Kanye West vimeuzwa kwa $1.8m (£1.3m) katika mnada ikiwa ni bei ya juu zaidi kuwahi kununuliwa .
Viatu hivyo aina ya Nike Air Yeezy 1vilivunja rekodi iliowekwa na viatu vya Nike Air Jordan 1s vilivyouzwa kwa $615,000 mwaka uliopita.
Mauzo hayo pia yanamaanisha kwamba ndio viatu vya kwanza aina ya sneakers kuuzwa kwa bei ya juu ya $1m," lilisema jumba la minada la Sotheby siku ya Jumatatu.
Kanye West kwa mara ya kwanza alivalia viatu hivyo katika tamasha la Grammy mwaka 2008 .Viatu hiyo ni saizi 12 au 11 ya Uingereza.
Vilinunuliwa na RARES, mtandao wa kuwekeza viatu visivyo vya kawaida.
Wanachama wake wanaweza kununua hisa katika viatu sawa na jinsi wawekezaji hununua hisa katika kampuni.
Viliuzwa na aliyevichukua viatu hivyo Ryam Chang katika mauzo ya faragha, ikimaanisha kwamba mnunuzi na bei yake haiwezi kuchapishwa hadi mnunuzi atakapokubali kujitokeza.
‘’Mauzo hayo yanaadhimisha bei ya juu kuwahi kuchapishwa hadharani ‘’,ulisema mnada huo katika taarifa yake.