"Tarehe 8 Aprili 2021, vijana wa Jeshi la kujenga Taifa wapatao 854 ambao ni miongoni mwa vijana 2,400, walio haidiwa kupewa ajira na Mhe. Rais kwa kutekeleza ujenzi wa ofisi za ikulu ya Chamwino waliamua kugoma, kukataa kufanya Kazi eneo jingine na kuandamana kwenda Ikulu kumuona Mhe. Rais kushinikiza kuandikishwa Jeshi.
Mkuu wa Jeshi la kujenga Taifa Meja Jenerali Charles Mbunge kawasihi kusitisha mgomo huo na kutoandamana hawakusikiliza, kitendo hiki haikikubaliki, kugoma au kuandamana Jeshini ni kosa la Uasi , wangekua askari wangefikishwa mahakamani kwa sababu hiyo Jeshi la kujenga Taifa limesitisha mkataba wa vijana hao 854 wa kujitolea na kurudishwa makwao." Jen. Mabeyo
VIDEO: