Video ya polisi akimshambulia kwa risasi kijana wa miaka 13 yatolewa Chicago





Polisi wa Chicago wametoa picha za afisa aliyempiga risasi mtoto wa miaka 13 kwenye uchochoro wa giza.
Video hiyo inaonesha polisi huyo akipiga kelele "dondosha" kabla ya kumpiga risasi Adam Toledo mara moja kifuani tarehe 29 mwezi Machi.

Mvulana haonekani kuwa ameshika silaha katika sekunde ya pili alipigwa risasi, lakini video ya polisi inaonesha bunduki karibu na mahali alipoangukia.

Maandamano madogo yalifanyika Alhamisi jioni karibu na Chicago, saa kadhaa baada ya meya wa jiji hilo kuomba utulivu.

Kutolewa kwa video hiyo kunafuatia tukio baya la polisi kufyatua risasi tarehe 11 Aprili dhidi Daunte Wright na afisa katika kitongoji cha Minneapolis.

Upigaji risasi huo umesababisha maandamano makali wakati jiji linasubiri matokeo ya kesi ya Derek Chauvin, afisa anayeshtakiwa kwa kifo cha George Floyd.

Kipande hicho kinaonesha afisa huyo akiruka kutoka kwenye gari la kikosi chake na kumfukuza kijana huyo wa Latino kwa miguu chini kwenye uchochoro wenye giza wakati mtuhumiwa mwingine akipotea machoni.

Polisi huyo anapiga kelele: "Polisi! Simama! Simama sawa sasa hivi! Mikono! Mikono! Nioneshe mikono yako!"

Mvulana anageuka na kuinua mikono yake. Afisa anapiga kelele "Achia" na anapiga risasi - sekunde 19 baada ya kutoka kwenye gari la kikosi chake.

Picha tofauti za CCTV zinaonekana kuonesha kijana huyo akitupa kitu kwenye upenyo wa uzio wakati afisa huyo anamkimbilia. Video ya inaonesha maafisa wakimulika taa silaha nyuma ya uzio wa mbao baada ya ufyatuaji risasi.

Polisi huyo anaita gari la wagonjwa huku akimsihi kijana aliyeanguka "kuwa macho". Maafisa wengine wanafika katika eneo hilo katika kitongoji cha Little Village upande wa magharibi mwa jiji na hatua ya kurejesha mapigo yake ya moyo (CPR) inafanywa.

Kulingana na waendesha mashtaka, kijana huyo alikuwa na mtu wa miaka 21, Ruben Roman, ambaye alikuwa amefyatua bunduki kwenye gari lililokuwa likipita. Milio ya risasi iliwavuta polisi katika eneo hilo, na kusababisha makabiliano makali.

Bwana Roman alijitokeza mahakamani Jumamosi akishtakiwa kwa utumiaji mbaya wa silaha, utapeli wa silaha na kuhatarisha maisha ya watoto, kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari.

Ofisi ya Uraia ya Uwajibikaji wa Polisi ilitoa picha za kamera siku ya Alhamisi pamoja na video ya CCTV, ripoti za kukamatwa na rekodi za sauti za risasi zilizopigwa katika eneo hilo ambalo liliwajulisha polisi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad