Waliochanjwa Corona tu Ndio Wataruhusiwa Kuhiji Mecca





Mamlaka za nchini Saudi Arabia zimesema watu waliopata chanjo ya corona peke yake ndio wataruhusiwa kufanya ibada ya Hija mwaka huu huko Mecca.

 

 

Wizara ya Hija na Umrah imetoa taarifa kuwa watu waliopata chanjo pekee ndio watakuwa na vigezo vya kujihi mwaka huu katika mji mtakatifu wa Mecca.

 

 

“Watu ambao tayari wamepata chanjo dozi mbili za COVID-19, na wale ambao wamepata chanjo dozi moja ya corona siku 14 kabla ya Hija au mtu ambaye ametoka kupona corona”, wizara imesema.

 

 

Wizara hiyo imesema pia kuwa itazingatia taratibu zote za kujikinga dhidi ya maambukizi ya corona. Haijawekwa wazi kama sera hiyo itaendelea mpaka wakati wa Hija kuu baadae mwaka huu.

 

 

Saudi Arabia imeripoti kuwa na maambukizi ya virusi vya corona zaidi vya zaidi ya watu 393,000 na zaidi ya vifo 6,700 vinavyotokana na virusi hivyo.

 

 

Wizara ya afya ya taifa hilo imesema watu zaidi ya milioni tano wamepata chanjo dhidi ya corona, katika taifa lenye watu zaidi ya milioni 34.

 

 

Mwezi uliopita mfalme Salman alimbadilisha waziri wa Hija , alafu mwezi mmoja baadae ilifanyika Hija ndogo katika mfumo mpya wa kihistoria kutokana na changamoto ya virusi vya corona.

 

 

Mwaka jana, waislamu 10,000 ambao ni wakazi wa Saudi Arabia ndio waliruhusiwa katika Hija takatifu mwaka jana,ingawa mara zote huwa ni watu milioni 2.5 kutoka duniani kote na ndio walishiriki mwaka 2019.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad