Wanandoa kutoka Taiwan wamekua gumzo hususan katika mitandao ya kijamii baada ya kuoana mara nne katika kipindi cha mwezi mmoja.
Hadithi hii ambayo iliwashangaza wengi, ilithibitishwa na Wizara ya kazi ya Taiwan.
Makampuni ya Taiwan hutoa siku 8 za mapumziko kwa wanandoa wapya , lakini mfanyakazi mmoja wa benki aliamua kudai siku 32 kwa kuoa mara nne, jambo ambalo sio la kawaida nchini humo.
Katika kipindi cha siku 37 , yeye na mke wake walioana mara nne na kuachana mara tatu, wakidai siku nane kwa kila ndoa.
Mfanyakazi huyo wa benki moja ya Taiwan alikata rufaa katika mahakama ya jiji la Taipei ya masuala ya wafanyakazi, ambayo hatimaye ilimtoza faini muajiri wake ya Tw$20,000 pesa za Taiwan ( sawa na dola 670) kwa kukiuka sheria za likizo ya mfanayakazi huyo.
Hiyo ni kwasababu kulingana na sheria iliyopo, hakuna masharti yoyote yanayoelezea ni mara ngapi mtu anapaswa kuomba likizo kwa ajili ya kufunga ndoa.
Benki iliyomuajiri mfanyakazi huyo, ambayo ilikuwa tayari kumpatia siku nane tu za likizo ya kuoa, ilisema mwanaume huyo alikuwa "ametumia vibaya" sheria.
Kesi hiyo imeibua ukosoaji mkubwa katika mtandao dhidi ya mfanyakazi huyo wa benki kwa kutumia mapungufu ya sheria na kwa idara ya kazi kwa kutoza faini.
"Siamini, huyu mwanaume ni kama anacheze unyumba kwa ndoa na talaka zake. Itakuaje kama anataka kuoa na kutaliki kila siku? Anafaa kupewa likizo ya ugonjwa kuliko likizo ya uzazi ," uliandikwa mmoja wa ujumbe wa mtandao wa kijamii.
Wiki iliyopita idara ya Wafanyakazi iliondoa fine dhidi ya benki "kutambua kosa na kuboresha," kulingana na taarifa yake.
Kana kwamba haitoshi, mwanaume huyo , ambaye aliacha kazi katika benki hiyo, aliipigia simu Idara ya wafanyakazi kulalamika kwamba anamdai muajiri wake wa zamani siku 24 za likizo, afisa ambaye hakutaka jina lake litajwe ameliambia shirika la habari la AFP.
Tukio hilo limekuwa likilinganishwa na kile kinachoitwa "salmon chaos" kilichoelea Taiwan mwezi uliopita kuhusu mamia ya watu, wengi wao wakiwa ni vijana, waliobadilisha majina yao halisi na kuitwa "Gui Yu" au salmon.
Kubadilishwa kwa jina na mtu Taiwan ni jambo rahisi na wale wanaochukua hatua hiyo walitumia fursa ya mgahawa uliokuwa ukinadi chai yake na kutoa chai ya bure kwa yeyote aliyekuwa na jina salmon kati ya majina yake.
Baadhi ya watu waliochagua jina salmon walichagua kuitwa "Salmon Prince", "Salmon Fried Rice" na "Bao Cheng Gui Yu" — yanayoweza kumaanisha, Salmon mwenye muonekano wa mvuto wa kupindukia.