Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amesema wamekuja na mkakati wa kuwakamata na kuwawezesha Wanawake wanaofanya biashara ya ngono kwa kuwaweka katika eneo moja lililopo Chanika ili waweze kufanya shughuli za kilimo na ufugaji
Biashara hiyo imeonekana kushika kasi Wilayani Ilala na ugumu wa maisha umetajwa kuwa sababu kubwa ya Wanawake hao kufanya vitendo hivyo
Amesema mkakati huo unalenga kudhibiti biashara hiyo ambayo ni kinyume na maadili ya Watanzania, na Wanawake watapata fursa ya kutengeneza fedha kihalali na kujijenga kiuchumi
Kwa mujibu wa DC Mjema, wapo mbioni kukamilisha taratibu za kuandaa eneo hilo na utakapokamilika, Wanawake watakaokamatwa watafikishwa hapo moja kwa moja na kufundishwa mbinu za kujiendeleza