Wapiganaji wa upinzani wakiwa na silaha kali walijiweka katika hali ya utayari katika sehemu mbalimbali za mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, Jumatatu. Hali hii imetokea ikiwa ni siku moja baada ya kuzuka kwa mapigano dhidi ya vikosi vya serekali kupinga hatua ya kuongezewa muda kwa rais, katika nchi ambayo imekumbwa na ghasia kwa miaka mingi. Wapiganaji hao waliweka vizuizi katika barabara huku watu wenye silaha pamoja na magari yakiwa na bunduki za risasi za rashasha waliwekwa katika ngome za upinzani baada ya mapigano yaliyo sababisha vifo vya watu watatu. Shuhuda mmoja aliyetambulika kwa jina la Abdullahi Mire, na kuzungumza na shirika la habari la AFP, amesema kwamba vikosi vyote vya wapiganaji wa serekali na upinzani wote wamejiweka tayari katika barabara muhimu za mji.