WATU 15 wamefariki baada ya moto kuzuka kutokana na mitungi ya gesi ya Oksijeni kulipuka katika hospitali ya Ibn al-Khatib Baghdad nchini Iraq ambayo inahudumioa wagonjwa wa Covid 19.
Vikosi vya zimamoto, walikimbia kuuzima moto na kuwaondoa wagonjwa katika hospitali ya Ibn al-Khatib, ambayo hutoa huduma kwa wagonjwa mahututi walio na maambukizi ya Corona.
Ripoti za awali kutoka kwa matabibu na maafisa wa usalama zinaashiria kuwa watu wasiopungua 36 wamejeruhiwa.
Iraq inakabiliwa na wimbi kali la maambukizo ya Covid 19, huku maambukizo mapya kwa siku yakifikia watu takriban 8,000 idadi kubwa zaidi tangu kuzuka kwa janga hili.
Serikali imekua ikihimiza umma kupata chanjo, lakini idadi ndogo inajitokeza kwa sababu ya kutoamini mfumo wa huduma za afya na chanjo yenyewe.