Waziri wa TAMISEMI Ummy Mwalimu @ummymwalimu amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema Magesa Boniphace kuanzia leo April 20,2021 kupisha uchunguzi dhidi yake.
Waziri Ummy amechukua hatua hiyo baada ya kupokea malalamiko ya tuhuma za ubadhirifu wa fedha za miradi ya maendeleo katika Halmashauri hiyo kutoka kwa Wananchi na Viongozi mbalimbali akiwemo Mbunge wa Jimbo hilo Hamisi Tabasamu.