Mtawala wa Cambridge na Mtawala wa Sussex walionekana wakizungumza pamoja wakati wanaondoka katika mazishi ya babu yao, Mtawala wa Edinburgh.
Kaka hao walizungumza wakati wanaondoka kanisa la St George huko Windsor, wakiwa pamoja na Mke wa Mtawal wa Cambridge.
Ikiwa ni mara ya kwanza wawili hao kukutana tangu Mwanamfalme Harry alipoacha rasmi majukumu ya kifalme zaidi ya mwaka mmoja uliopita.
Mwezi uliopita, Mwanamfalme Harry alidokeza kuwa wanatoafauti zao kati yake na kaka yake Mwanamfalme William.
Katika mahojiano na Oprah, alisema kuwa wawili hao wazo katika “njia tofauti”, na kwamba “uhusiano wao haukuwa vizuri wakati huo”
Hata hivyo, Jumamosi, wana hao wa kifalme walionekana hadharani wakitembea pamoha huku na binamu yao Peter Phillips akiwa katikati yao wakiwa nyuma ya jeneza la babu yao wakati linapelekwa kanisani.
Ilikuwa ni karibu miaka 24 tangu kaka hao wawili walipoonekana wakitembea namna hiyo pamoja katika mazishi ya mama yao, Diana, Mwanamfalme wa Wales.
Mwanamflame William na Mwanamfalme Harry wakitembea pamoja na binamu yao Peter Phillips, ambaye alirudi nyuma yao kidogo
Mwanamflame William na Mwanamfalme Harry wakitembea pamoja na binamu yao Peter Phillips, ambaye alirudi nyuma yao kidogo
Katika ibada ya mazishi, watu 30 pekee ndio waliokuwepo ambao walikuwa wamevaa barakoa na pia walitekeleza hatua ya kutokaribiana kuendana na masharti ya kukabiliana na virusi vya corona, huku Malkia akiwa ameketi peke yake.
Pia aliyekuwa ameketi peke yake ni Mwanamfalme Harry aliyekuwa mkabala wa njia na kaka yake na dada mkwe wake Catherine.
Mke wa mwanamfalme Harry, Meghan, ambaye ni mjamzito na mtoto wao wa pili, hakuhudhuria mazishi hayo kwa ushauri wa daktari wake na badala yake alikuwa nyumbani kwao California.
Huduma hiyo, iliyoendeshwa na kiongozi wa Windsor, ilitoa heshima za mwisho kwa Mwanamfalme Philip na kumshukuru kwa “ukarimu, ucheshi, na utu wake” kwa “namna mbalimbali maisha yake yamekuwa baraka kwetu”.
Aerial view of Windsor Castle
Njia ya msafara wa jeneza litakaoubeba mwili wa Mwanamfalme Philip
Uhusiano wa mtawala huyo na jeshi la majini na upendo wake wa maji uliangaziwa pakubwa,huku wimbo wa ‘Eternal Father’ wa mwaka 1860, Strong to Save ulioimbwa na William Whiting ikiimbwa.
including through the 1860 hymn Eternal Father, Strong to Save, by William Whiting.
Baada ya sherehe hiyo, mwanamfalme Harry aliungana na Mwanamfalme William na Catherine wakati wanaondoka kanisani. Watatu hao walikuwa wakizungumza kwa pamoja wakielekea eneo kuu la kasri.
The Duchess of Cambridge
Sawa na wake wengine wa kifalme, Mke wa Mtawala wa Cambridge hakuwa sehemu ya msafara wa kabla ya mazishi badala yake alienda kanisani kwa kutumia gari
Meghan na Mwanamfalme Harry walituma maua yao yaliyojumuisha maua ya taifa ya Ugiriki, kuwakilisha urithi wa Mwanamfalme Philip, na mmea maalum wa baharini kuwakilisha wanajeshi wa majini wa familia ya Kifalme.
Kadi iliyokuwa kwenye maua ilikuwa imeandikwa kwa mkono na Meghan, ambaye ni stadi wa maandishi ya kaligrafia ambaye pia alikuwa akiandika kwenye kadi za mwaliko wa harusi.