Yanga kuwakosa nyota watatu dhidi ya TZ Prisons leo





Msemaji klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli amethibitisha kuwakosa wachezaji nyota watatu wa kikosi cha kwanza kwenye mchezo wa mtoano wa 16 bora wa kombe la Shirikisho dhidi ya TZ Prisons utakaochezwa saa 10:00 jioni ya leo kwenye uwanja wa Nelson Mandela mkoani Rukwa.
Wachezaji hao watakaokosekana ni viungo wa kati,Tonombe Mukoko, Feisal Salum “Fei Toto” na mshambuliaji Michael Sarpong baada ya wachezaji hao kuoneshwa kadi za manjano tatu mfululizo hivyo kutumikia adhabu ya kukosa mchezo mmoja.

Benchi la ufundi la Yanga linaloongozwa na kocha wake mpya, Mtunisia, Mohammed Nasruddine Nabi linatazamiwa kuwageukia viungo Zawadi Mauya kuchukua nafasi ya Tonombe Mukoko,Carlinhos kucheza nafasi ya Fei Toto na Ditram Nchimbi kama mbadala wa Sarpong.

Kwa upande wa nahodha wa Prisons, Benjamin Asukile amejinasibu kuwaondoa Yanga na kutinga robo fainali kwasababu wamejiandaa vya kutosha ukizingatia na kusema wana uwezo wa kufanya hivyo tena kwenye dimba lao la nyumbani.

Ikumbukwe kuwa, kwenye michezo miwili ya VPL msimu huu, Yanga na TZ Prisons wametoka sare ya bao 1-1 kwenye michezo hiyo huku ikishuhudiwa kuwa yenye upinzani huku moja ya sababu ikiwa ni TZ Prisons kucheza mchezo wa mabavu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad