Yanga Wamtambulisha Kocha Mpya, Atinga Na Mkalimani Wake





KOCHA Mpya wa Yanga raia wa Tunissia, Nasreddine Nabi baada ya kutambulishwa rasmi leo Aprili 20 kuchukua mikoba ya Cedric Kaze aliyefutwa kazi Machi 7 kutokana na mwendo mbovu wa timu hiyo mzunguko wa pili amesema kuwa yeye ni kocha wa vitendo hapendi porojo.

Mbele ya Waandishi wa Habari katika mkutano wa utambulisho wa Mtunisia huyo ameweka wazi kwamba anaitambua Yanga kwa kuwa alikuwa anaifuatilia muda mrefu jambo ambalo halimpi tabu.



Ataungana na mzawa Juma Mwambusi ambaye kwa sasa anainoa Yanga akiwa ni Kaimu Kocha Mkuu ambapo wambusi ataongoza mchezo wa leo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Gwambina FC utakaochezwa Uwanja wa Mkapa, saa 1:00 usiku.

Kocha huyo amesema:”Mimi ni kocha wa vitendo, sipendi porojo wala bla bla bla hapana kwangu ni kazi nataka Yanga iwe timu kubwa.

“Ninaijua vizuri na nina amini kwamba nitafanya vizuri hivyo ninashukuru kwa nafasi ambayo nimeipata nitatoa ushirikiano na kufanya kazi kwa ufanisi,” amesema.



Yanga kwenye msimamo ipo nafasi ya kwanza ikiwa imecheza jumla ya mechi 25 na kukusanya pointi 54, leo inakutana na Gwambina FC iliyo nafasi ya 12 kwenye msimamo na pointi 30 na imecheza mechi 24.

Kocha huyo ana uzoefu na soka la Afrika kwa kuwa miongoni mwa timu ambazo alifundisha ni pamoja na Al Merrikh ya Sudan ambayo iliishia hatua ya makundi, Ligi ya Mabingwa Afrika.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad