Zifahamu Rekodi Kali Alizovunja Rapa DMX






Rapa DMX alikuwa miongoni mwa nyota waliofanikiwa sana nchini Marekani mwishoni mwa miaka ya 1990 mpaka miaka ya 2000, na mafanikio yake aliyapata kupitia historia aliyoiweka katika muziki baada ya kuwa msanii wa kwanza kuona albamu zake tano za kwanza kuwa namba moja katika chati za muziki bora za Billboard.

 

 

 

Waliuza rekodi milioni 14 nchini Marekani na kumuwezesha kuchaguliwa katika tuzo za Grammy mara tatu , na alifurahia tasnia yake ya nyota wa filamu.

 

 

Siri ya muziki wa DMX kupendwa na wengi ni kutokana na upekee wake wa kuweza kufanya muziki wake kuwa wa kibiashara wakati huohuo akiendeleza mtindo wake wa kuimba kwa kufokafoka katika ubora wa kiwango cha juu.

 



Umahiri katika maonesho yake yalikuwa yanadhihirisha ubora wa kazi yake , kuanzia kuonesha misuli na michoro ya tatoo na sauti yake ya kufokafoka wakati akiimba.

 

Lakini DMX alikuwa makini sana katika kujiandaa katika maonesho yake ambapo mtindo wake ulikuwa hautabiriki.

Mistari ya nyimbo zake inaweza kubadilika kutoka kwenye maumivu, masuala ya kiroho na masuala ya uhalisia wa maisha mtaani.



 

Kwa miaka mingi, muziki wa DMX umekuwa wa mihemko zaidi na unaotoa majibizano ya hisia zake zake, na changamoto ambazo alikuwa nazo ambazo zilipelekea kuwa mraibu wa dawa za kulevya, kukaa kwenye nyumba za kujirekebisha na matumizi ya dawa za kulevya(rehab), kukamatwa mara kadhaa na kufungwa kutokana na makosa yanayohusisha dawa za kulevya , ukwepaji wa kodi, kuwa na silaha bila kibali na ukatili wa wanyama.

 

 

Katika mahojiano aliyofanya mwaka 2020 akiwa na rapa na wanaharakati wenzie , DMX alisema jinsi alivyoanza kuwa mraibu akiwa na umri wa miaka 14 wakati mwalimu aliyekuwa akimfundisha muziki ambaye alikuwa ana miaka 30 wakati huo alipompa bangi na mpaka alipofikia kutumia cocaine.

 



“Mwanaume huyu, Mwanaume huyu, mwanaume huyu… aliniingiza kwenye sehemu ya mafanikio ya maisha yangu ambayo ni muziki, lakini alinipitisha katika changamoto ambayo inanitesa,” alisema DMX.

 

 

“Baadae niligundua kuwa alikuwa ananiwekea na dawa za kulevya. Kwanini ufanye vitu kama hivyo kwa mtoto? Alikuwa na miaka 30 na alifahamu kuwa ninamwamini. Unafanyaje vitu kama hivyo kwa mtu ambaye anakuangalia wewe na kukutegemea?”

 

 

Mwanzo mgumu
DMX ambaye jina lake la kuzaliwa ni Earl Simmons alizaliwa mwezi Desemba, tarehe 18 mwaka 1970, na alikuwa katika mji wa Mount Vernon, New York.

 

 

Unyanyasaji na maisha magumu aliyopitia wakati wa utoto wake katika nyumba ya malezi yalipelekea kujihusisha katika ghasia na uhalifu hivyo kukamatwa na polisi mara kadhaa na alikamatwa na polisi mara ya kwanza akiwa na miaka 15.

 

 

Maisha hayo ya tabu aliyopitia aliyaeleza wazi katika tungo zake za maisha ya gheto. DMX alifahamika kupenda mbwa na hata alichora tatoo ya mbwa wake Boomer, alipogongwa na gari na kufa.

 

 

DMX aitumia mara nyingi taswira za mbwa katika tungo zake kama kwenye wimbo wake wa kwanza wa ‘ Get At Me Dog’ iliotoka mwaka 1998. Wimbo huo ulitamba kwa muda mrefu na kuingia kwenye chati za Billboard na kuwa namba moja.

 

 

Mwaka huohuoalitoa wimbo wa ‘Slippin’ ambao ulizungumzia magumu ambayo alipita rapa huyo katika maisha yake na wimbo huo ulipigwa mahakamani kabla ya mwmbaji huyo hajahukumiwa kwa kukwepa kulipa kodi mwaka 2018.

 



“Maisha aliyopitia yalikuwa mbaya mno,” wakili wake Murray Richman alisema. “Nimesikia simulizi nyingi lakini sijawahi kusikia mtu akiwa amekulia katika malezi mabaya kama haya.”

 

 

DMX alianza kupata faraja katika hip-hop, alianza kama DJ na baadae akaanza kuimba kwa kufokfoka, na kujipatia jina la DMX (Dark Man X).

 

 

Alikuwa hafahamiki aliposaini rekodi za Columbia mwaka 1992, rapa huyo hakupata fursa kubwa alipopewa nafasi ya kutangaza wimbo wake wa ‘Born Loser came and went unnoticed’.

 

 

DMX alilalamikia lebo hiyo kumpuuzia na aliondoka bila kumaliza mkataba wake. Alitengeneza wimbo mwingine mwaka 1994, Make A Move, lakini alikamatwa kwa kutumia dawa za kulevya mwaka huohuo.

 



Alianza kutamba
Alianza kujenga kipaji chake kwa kuimba na wasanii wengine kama LL Cool J’s 4, 3, 2, 1 na Mase katika wimbo wa 24 Hours To Live.

 

 

Na akaja na wimbo wa It’s Dark And Hell Is Hot, ambao ulimfanya afananishe na hayati Tupac Shakur kutokana na uimbaji wake.

 

 

“Nadhani jamii iko tayari kukabiliana na uhalisia,” aliripotiwa kuiambia Def Jam Records mwaka 1998. “Kwasababu hiyo sina namna nyingine zaidi ya kutamba tu!”

 

 

Si muda mrefu tangu azindue albamu yake , alishutumiwa kubaka lakini baadae kesi hiyo alishinda baada ya ushahidi wa DNA kuonesha si kweli.

 

 

Alienda akashiriki kwenye filamu ya debut in Hype Williams’ akiwa mtu mwenye malengo lakini bila mafanikio , jambo ambalo alikosolewa kwa migogoro yake. DMX alikuwa anafanyia kazi albamu yake ya pili ya Flesh of My Flesh, Blood of My Blood.



 

Ilikuwa na picha ambazo hazikueleweka zikiwa na damu -lakini mashabiki wake walifanya albamu hiyo kuwa juu katika chati.

 

 

“Nilitaka kusema kile kilichokuwa katika fikra zangu na kuelezea maumivu yangu yote.Nimejifunza kuwa nikiyatoa naeleleweka na ulimwengu.”

 

 

Kwa mafanikio ya albamu zake, DMX alikuwa msanii wa kwanza wa rap kuwa katika chati za muziki bora Marekani ndani ya mwaka mmoja. “Niliandika haraka,” DMX aliiambia MTV mwaka 1999.

 

 

Mwaka huo alijumuika katika ziara ya wanamuziki wengine maarufu kina Jay-Z, Method Man, na Redman, na kuanzisha kundi Jay-Z na Ja Rule. Pia alizindua wimbo kama Ruff Ryders’ Anthem, What’s My Name, Party Up (Up In Here), na Who We Be, na baadae miwili kati ya hiyo ilichaguliwa katika tuzo za Grammy-.



 

Wakati DMX aking’arisha kipaji chake cha uimbaji alianza kujitangaza katika vipaji vingine. Alishiriki filamu ya Romeo Must Die, akiwa na Jet Li na Aaliyah mwaka 2000, na filamu ya Exit Wounds, akiwa na Steven Seagal mwaka 2001.

 

 

Walicheza tena filamu na Li mwaka 2003 ya Cradle 2 The Grave. Huku akiendeleza muziki wake na mwaka 2006 alizindua albamu yake ya Year Of The Dog… na Undisputed mwaka 2012.

 

 

Lakini vita yake na dawa za kulevya iliendelea kuwa jinamizi kwake na kusababishwa kukamatwa kutokana na matumizi ya dawa za kulevya na umiliki wa silaha.

 

 

Mwaka 2001, alitumikia kifungo cha siku 15-kwa kuendesha bila ya kuwa na leseni wakati aliposhutumiwa kumtukana mlinzi. Masuala ya afya ya akili yalikuwa mada katika mahojiano aliyofanya.



 

Alisema X haimuwakilishi yeye.

“X ni mwanaume mbaya. Huyo si mimi.Mimi sio mtu ambaye vyombo vya habari vinanitafsiri kuwa,” alisema. “Nilikuwa wazi ya kuwa mimi ni nani na wasifu au tabia zangu.

“Lakini sifahamu. Mpaka hapa , sina uhakika hata na utofauti wake.

 



Mimi ni Earl nilipokuwa na watoto wenzangu . Ninawakumbuka watoto wangu.” Rapa huyo ana watoto 15 kutoka mahusiano tofauti.Alikuwa amemuoa Tashera Simmons mwaka 1999 na walioana kwa miaka 11 na waliendelea kuwa marafiki.

 

 

Mwaka 2016, DMX alizirahi kwa kutumia dawa kupita kiasi na kuegesha gari mara nyingi katika hoteli za New York. Mwaka uliofuata alisitisha maonesho yake na kwenda rehab tena. “Ni muhimu sasa kuchukua muda kuangalia afya yangu ili niwe baba bora ,rafiki na mtoa burudani bora,” meneja wake Pat Gallo alisema.



 

Alikamatwa kwa kukwepa kodi mwaka 2018, kwa kushindwa kulipa dola ya milioni 1.7 alizopata mwaka 2002 na 2005. Na alishindwa kulipa kodi kutoka mwaka 2010 mpaka 2015, alipokadiriwa kupata dola milioni 2.3.

 

 

Jaji alidai kuwa huo ni utapeli wa kodi na kumfunga mwaka mmoja gerezani . Baada ya kuachiwa huru mwaka 2019, DMX alirudi rehab tena.



 

Katika mahojiano yake na Talib Kweli, DMX alisema amejifunza kuwa ni muhimu kupona na kuwa muwazi katika matatizo yake na kutoogopa kuomba watu wamsaidie.

 

 

“Nimejifunza kuwa napaswa kukabiliana na vitu vinavyoniumiza,” rapa huyo alisema.

“Sina mtu wa kuongea naye…

“Kuongea kuhusu matatizo yako kunatazamwa kama ishara ya udhaifu wakati ni jambo la ujasiri ambalo unaweza kufanya .”

 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad