Aliyemuua Mkewe, Amuua Mke Mwingine Tena




Mahakama Kuu Kanda ya Tabora imemuhukumu kutumikia kifungo cha kwenda jela miaka minne Lameck Essau Meza mkazi wa Sikonge mwenye umri wa miaka 38 baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumuua bila kukusudia mkewe Dafroza Paul.

 

Akisoma hukumu hiyo Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, Amour Khamis amesema baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili katika shauri hilo la mauaji namba 19 la mwaka 2017, mahakama imejiridhisha pasina shaka yoyote kwamba mshtakiwa Lameck alifanya tukio hilo la kumpiga mkewe na kusababisha kifo chake kinyume na kifungu cha 196 Disemba 24 mwaka 2012 huko Kijiji cha Mwenge wilayani Sikonge.

 

Hata hivyo kabla ya kutolewa hukumu Upande wa Jamhuri ulidai kuwa mshtakiwa hii ni mara yake ya pili kufanya mauaji ya aina hiyo ambapo awali alimuua mke wake wa kwanza na kufikishwa mahakamani akahukumiwa kwenda jela miaka minne baada ya kupatikana na hatia ya kuua bila kukusudia na hii ilikuwa ni mara yake ya pili kurejea kosa la aina hiyo baada ya kumuua mkewe huyu mwingine.

 

“Hii ni mara ya pili alishawahi kumuua bila kukusudia Mkewe wa kwanza (kwa kumpiga) na alihukumiwa kifungo cha miaka minne pia,” ilielezwa mahakama hiyo.

 

Jaji mfawidhi wa mahakama hiyo kuu kanda ya Tabora alidai kuwa mauaji hayo ameyafanya tena bila kukusudia kutokana na hasira za ghafla za mshtakiwa zilizotokana na mwanamke huyo kuchelewa kurudi nyumbani na ndipo akawa anamuonya kwa kumpiga mateke, ngumi na vipande vya tofali.

 

Lameck Meza amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka minne Jela huku mahakama ikiacha milango wazi ya kukata rufaa.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad