Aning’inia kwenye daraja refu baada ya sehemu ya daraja kuvunjika


 
Mwanaume mmoja alibaki akining’inia kwenye daraja baada ya moja ya paneli zake zilizotengenezwa kwa kioo kuharibiwa kutokana na upepo mkali.



Mtu huyo alikuwa akitembelea kwenye daraja la urefu wa mita 100 kwenda juu katika mlima wa Piyan, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo wakati tukio hilo lilipotokea siku ya Ijumaa.

Vipande kadhaa vya sakafu ya kioo ya daraja vilivunjwa na upepo makali uliosafiri kwa kasi ya 150km kwa saa.

Inafikiriwa kuwa China ina karibu madaraja 2,300 na maeneo mengine ya barabara kupita.

Maeneo hayo yametengenezwa ili kuvutia watalii na kukuza utalii wa ndani wa China.

Picha ya tukio hilo ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionesha mtu huyo akiwa amening’inia katikati ya daraja, lililokuwa katika eneo la karibu na mji wa Longjing.

Kikosi cha zimamoto lilikimbilia eneo la tukio ili kumuokoa mtu huyo. Hatahivyo aliweza kutolewa akiwa salama, Shirika la habari nchini humo Xinhua limeripoti.

Mtalii huyo alipelekwa hospitali kwa ajili ya uchunguzi na ushauri nasaha, na sasa inaelezwa kuwa yuko vizuri kimwili na kiakili”.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad