Ikiwa Bado Kuna Mdahalo Mrefu sana Kuhusu Kazi za Wasanii Kupitiwa na Baraza la Sanaa Nchini Tanzania (BASATA) Kabla Hazijatoka
Wasanii wameanza Kulivalia njuga Swala Hili na Wengi wakiwa hawajaunga Mkono kwa kuandika Katika Mitandao ya Kijamii na Kuzungumza Katika Vyombo vya Habari
Baada ya @mwanafa Kuandika Ujumbe Akipingana na Swala Hili ... @aytanzania na yeye ameandika Ujumbe Katika Comment ya Post ya Mwana FA akiongezea kuwa BASATA Wamekua na Tabia ya Kukagua Nyimbo za Wasanii wa ndani tu na Nyimbo za Nje Kuendelea Kupewa Airtime kwenye Media
Hivyo anapingana pia na Utaratibu Huu Mpya akisisitiza kuwa Sio Sawa na Sio Haki kwa Msanii kutoa Wimbo kama Anafuatilia Maombi ya Visa ya North Korea
@aytanzania ameandika Kuwa 👇🏽
Basata wanakagua nyimbo za Tanzania peke yake tu na kuruhusu zingine za nje ya Bongo zipigwe hewani au? Kutoa wimbo kama unaomba Viza ya North Korea bwana SIO SAHIHI NA SI HAKI njia mbadala zipo nyingi tu