Babu Ajichimbia Kaburi na Kujenga Mnara, Anunuliwa Jeneza





Katika kile wengi wanaweza kuelezea kama jambo lisilokuwa la kawaida, mwanaume Mnigeria akiwa bado hai na buheri wa siha, Chifu Clement Usoro amejiandaa kwa kifo chake baada ya kujijengea kaburi na hata kusherehekea hafla hiyo kabla ya kuondoka kwake akisema hataki watoto wake kuandaa hafla ya mazishi baada ya kifo chake.

 

Mzee huyo mwenye umri wa miaka 73, katika mahojiano na BBC Pidgin, alisema alifanya maandalizi muhimu ya mazishi yake miaka mitatu iliyopita wakati alitimiza umri wa miaka 70. Kulingana naye, tayari ameandika wosia. Hata hivyo, Usoro, alisema anaendelea kuusahihisha kila wakati.

 

“Nimeandika wosia wangu na nitaendelea kuusahihisha kulingana na muda.Nimejenga kaburi langu. Ni kaburi lenye futi 9 kwa 9. Pia nimejenga mnara kando yake.

 

“Rafiki yangu alikwenda nami katika duka la jeneza kuona lenye nitapenda.Aliamua kuninunulia. Kama chifu, kuna mambo unatakiwa kufanya kabla ya kufa ama wafanye baada yako,” alisema Usoro.

 

Chifu Usoro pia alifichua kuwa amelipia vitu muhimu vya ibada kwa machifu wake wasaidizi akitoa ng’ombe ili kuwazuia wanawe kuwa na wasiwasi baada ya kifo chake.

 

Aliongezea kuwa hataki familia yake kuandaa hafla ya mazishi baada ya kifo chake akidai kuwa kusherehekea kifo chake ni kupoteza muda na pesa. Mzee huyo pia alisema aliwaagiza watoto wake kumzika siku tatu baada ya kifo chake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad