Mshambuliaji wa Manchester United na England Marcus Rashford amezungumza na aliyekuwa Rais wa Marekani Barrack Obama kuhusu jinsi vijana wanaweza kuchangia katika jamii.
Radhford , 23, aliongoza kampeni ya kukabiliana na uhaba wa chakula miongoni mwa Watoto mwaka uliopita wakati wa mlipuko wa virusi vya corona na kuteuliwa kuwa MBE .
Pia ameanzisha klabu ya vitabu itakayowasaidia watoto masikini kusoma zaidi.
”Vijana wengi ninaokutana nao, akiwemo Marcus wako mbele ya nilivyokuwa nilipokuwa na umri wa miaka 23”, alisema Obama.
”Tayari wanafanya mabadiliko na kuwa viongozi katika jamii zao”.
Obama mwenye umri wa miaka 59 na Rashford walizungumza kupitia njia ya ‘zoom call’ na pia walijadiliana kuhusu uzoefu wao, ikiwemo kulewa na wajane.
Radhford alisema kwamba sio jambo la kawaida kuzungumza na rais wa 44 wa Marekani akiwa ameketi jikoni. Lakini alinifanya nifurahi, aliongezea.
“Haikuchukua muda mrefu kabla ya kugundua jinsi uzoefu wetu ulivyolingana kama watoto katika kuwafanya walivyo wanaume unaowaona leo – shida, vizuizi na kila kitu.
“Kwa kweli nilifurahiya kila dakika yake. Wakati Rais Obama anazungumza, kile unachotakiwa kufanya ni kumsikiliza.”
L