Mechi ya watani wa jadi kati ya Simba na Yanga, uliopangwa kufanyika leo Jumamosi, kuanzia saa 1:00 jioni umehairishwa na Shirikisho la Soka Tanzania mpaka siku nyingine.
Mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara umeahirishwa kutokana na wachezaji wa Yanga na Benchi lao la Ufundi kuondoka katika uwanja wa Mkapa baada ya kuingia uwanjani saa 11:00 jioni na kusubiri kwa dakika 15 bila kumuona mpinzania wake, Simba uwanjani.
Awali mchezo ulipangwa kuanza saa 11 jioni lakini ulisogezwa hadi saa 1 usiku.
Wakati Yanga anaondoka, Simba nao wakaingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo tayari kwa kuingia uwanjani kukabiliana ya Yanga saa 1:00 usiku.