Jumatano wiki hii wimbo wa Childish Gambino "This Is America" ulitimiza miaka 3 tangu uachiwe rasmi na kuisumbua dunia ikiwemo kushinda tuzo 4 za Grammy 2019. Sasa Childish Gambino ameshtakiwa kwa madai ya kuiba wimbo huo.
Rapa mmoja aitwaye Emelike Nwosuocha maarufu kama Kidd Wes, ameibuka na kudai kwamba Gambino ameiba mistari, maudhui na muundo mzima kwenye wimbo wake ambao aliuachia Septemba 2016 kupitia SoundCloud na baadaye aliupandisha YouTube. Kisha alienda mbali zaidi kwa kuusajili kwenye ofisi za hakimiliki nchini Marekani mwaka 2017 akiuandaa kuwa wimbo wa kwanza kwenye album yake.
Kuthibitisha madai yake, Kidd Wes aliajiri mtaalamu wa masuala ya muziki (musicologist) ambaye alithibitisha madai ya Kidd baada ya kusikiliza nyimbo zote mbili. Nyaraka za mahakama zinasema. Hivyo Kidd Wes amefungua shtaka akidai fidia ikiwemo kukosa faida kwenye wimbo wake na pia fursa mbali mbali. Kwenye shtaka lake amewataja pia label ya RCA, Roc Nation na Young Thug aliyepiga back vocals.