Diamond Platnumz Ndio Mwanamuziki Bora Afrika Tukubali Tusikubali




Diamond ndiye Msanii Bora Afrika alianza kushikilia kijiti hiko kuanzia Mwaka 2016 mpaka sasa. Hata Wasanii wa huko Nigeria mnaowaona ni Bora wanalijua hilo
Wataalam wa Mambo wanasema "Numbers Dont Lie"

Kwanza anaongoza Afrika kwa Subscribers na Viwers YouTube tukiachana na hilo

Kila Msanii aliyewahi kumshirikisha Diamond basi wimbo huo ndio wenye Viewers wengi kuliko nyimbo zake zote alizowahi kufanya. Kama hauamini tafuta Nyimbo ambazo Diamond amewahi kushirikishwa na Wasanii Mbalimbali kisha angalia ni wimbo upi wa msanii huyo wenye Viewers wengi kuzidi aliomshirikisha Diamond, jibu utapata.

Davido alimshauri msanii King98 kuwa kama anataka kuhit afanye Colabo na Diamond Platnumz. Hii inaonesha wazi kuwa hata wasanii mnaowaona wakubwa Nigeria wanajua ukweli kuwa Diamond its a Best zaidi yao.

Wasanii mnaowaona wakubwa Nigeria kinachowabeba muda mwingine ni Lugha ya Kiingereza wanayoitumia ndio maana wanapewa nafasi kwenye Matamasha Makubwa lakini wanachokifanya ni kushika Suruali tu hawawezi Perfomance kumzidi Diamond Never labda Psquare ndio walikuwa zaidi enzi zao lakini sasa ni wakati wa Diamond hapa Afrika

Kila mtu anajua kuwa Diamond hana mpinzani Afrika kwenye Utumbuizaji, Diamond akipanda jukwaani Nchi yeyote Uwanja hulipukwa kwa Shangwe, Watu wanaenjoy Show hawachoki kutazama sababu Diamond anabadilika muda wote ana Ubunifu ambao hakuna anayeweza kuufanya. Anafanya Show ambayo ukiondoka hujutii Kiingilia chako. Sio kama wasanii wengine ni kushika Seruali tu na kuwaimbisha Mashabiki mwisho wa siku Mashabiki wanakuchoka.

Lakini Diamond hachoshi Perfomance anayoifanyaga ni zaidi ya Burudani hata Davido, Wizkid na Burnaboy hawafikii levo za Utumbuizaji wa Diamond, Diamond ni Michael Jackson wa Leo hana mpinzani Afrika ipo siku Dunia itasimama huyu mtu ni Next Level ni Jini la Muziki Afrika anastahili Heshima na tunaoweza kufanya aheshimike Afrika ni sisi wenyewe Watanzania.

Kuna msemo unasema "Nabii hakubaliki kwao" nasema ipo siku Mtamkubali tu Nabii.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad