DJ mkongwe zaidi astaafu akiwa na umri wa miaka 96




DJ wa miaka 96 huko Hong Kong ameandaa kipindi chake cha mwisho cha redio, baada ya zaidi ya miongo saba katika utangazaji.

Ray Cordeiro aliwashukuru wasikilizaji wake alipomaliza kipindi chake 'All The Way With Ray' Jumamosi usiku.

"Ndio hivyo. Asante sana kwa kuingia, kwaheri, asante kwa kuja," DJ huyo - anayejulikana kama Uncle Ray - alisema kwa Kiingereza na Kantonese.

Kipindi chake kimekuwa kikipeperushwa katika kituo cha kitaifa cha Hong Kong RTHK tangu 1970.

Cordeiro anajulikana kwa sauti yake nzito , kofia na nzuri ya muziki iliyowapendeza mashabiki wake

Mnamo 2000, Kitabu cha Guinness World of Records kilimpa jina la DJ 'aliyedumu' zaidi ulimwenguni.

Cordeiro, ambaye alizaliwa Hong Kong mwenye asili ya Ureno, alisema katika mahojiano ya hivi karibuni alikuwa "mtu mwenye bahati zaidi duniani".

"Kufanya kile ninachotaka kufanya, kupenda kile ninachotaka kupenda, na sidhani nina majuto yoyote," alikiambia kituo cha RTHK.

Wakati wa kazi yake hiyo kwa miaka 72, alitangamana na watu maarufu katika ulimwengu wa muziki, pamoja na Beatles, Cliff Richard na Tony Bennett.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad