Dk. Tulia apiga 'Stop' mijadala ya imani Bungeni

 


Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, amewataka wabunge kujitahidi kuacha kutoa mijadala inayohusu masuala ya imani za watu kwa sababu kila mtu anayo imani yake.

 

Kauli hiyo ameitoa leo Mei 17, 2021, Bungeni Dodoma, baada ya kuibuka mjadala uliohusu manabii wanaodai kuweza kufufua wafu, basi waweze kukaa pamoja na serikali ili kuweza kufanya jambo hilo, ambapo ameeleza kuwa serikali haina uwezo wa kutambua yupi ni nabii muongo na yupi ni mkweli.


"Mambo ya imani yataleta changamoto kidogo humu ndani, wale wananchi pengine kuna watu wao waliofufuliwa mimi sijui, hamna ndugu yangu aliyefufuliwa na huenda wapo na nisingependa Bunge letu lifike mahali tuanze kujadili imani za watu humu ndani," amesisitiza Dkt. Tulia.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad