Msanii wa Bongo Freva Abdulaziz Chende (26) maarufu Dogo Janja ameshikiliwa na jeshi la polisi na kuhojiwa akiwa na wenzie watatu.
Kamanda wa Polisi Viwanja vya Ndege ACP Jeremia Shilla amethibitisha kwamba Watu watatu akiwemo Abdulaziz Chende (26) maarufu Dogo Janja wamehojiwa na Jeshi la Polisi Kikosi cha Viwanja vya Ndege na kuachiwa wakituhumiwa kuwashawishi abiria wengine kukataa kufanya kipimo cha ugonjwa wa Covid-19 .