Miongoni mwa habari zilizotikisa wiki hii ni pamoja na dada wa staa wa Bongo Fleva Nasibu Abdul‘Diamond’ Esma Khan kumkataa hadharani aliyekuwa mume wa mwanamuziki Zuwena Mohammed ‘Shilole’ Ashraf uchebe.
Mrembo huyo mwenye watoto wawili wa kike, alisema kuwa Uchebe amekuwa akimfuatilia pale dukani kwake kwa muda mrefu lakini hawezi kuolewa na mwanaume ambaye hajielewi, ambaye muda wote anawaza ku –trendi tu.“
Mimi siwezi kuolewa na Uchebe, mwanaume gani kwanza yeye muda wote anawaza kutrend tu, yaani huyu Uchebe hana mapenzi ya kweli shida yake ni ku-trend tu huko mitandaoni sasa kwa hilo amefeli hawezi kunipata hata iweje”- alisema Esma
ZIMEANDALIWA NA MEMORISE RICHARD