Fisi wavamia makazi ya watu, waua mbuzi zaidi ya 10





 Fisi ambao idadi yao haijafahamika wamevamia makazi ya watu katika manispaa ya Shinyanga na kuua mifugo.
Kwa mujibu wa diwani wa Lubaga, Reuben Dotto, tukio hilo limetokea Mei 19, 2021 saa 10 alfajiri, akiitaja familia ya Monika Paul mkazi wa mtaa wa Azimio ambaye mbuzi wake 17 wameliwa na fisi hao.

Diwani huyo ameeleza kuwa  changamoto ya uwepo wa fisi kwenye maeneo yao imesababisha hofu kwa wananchi na baadhi ya wanafunzi kushindwa kwenda shule wakiwahofia fisi hao.

Baadhi ya wakazi wa eneo hilo waliozungumza na Mwananchi Digital wamesema kwa sasa fisi hao wanaonekana mara kwa mara katika maeneo yao tofauti na ilivyokuwa siku za nyuma, kuiomba Serikali iwasaidie.

Ofisa mifugo kata ya Lubaga,  Eliaremisa Mbise amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuagiza wakazi wa kata hiyo kuteketeza kwa moto  masalia ya mbuzi waliouawa na fisi ili kuzuia athari zinazoweza kujitokeza kutokana na baadhi ya wakazi wa eneo hilo kula mbuzi walioliwa na fisi.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad