Fred Vunjabei Ateuliwa Mwenyekiti Kamati ya Fedha UVCCM Taifa





Mfanya Biashara maarufu kama Fred Vunjabei jana tarehe 23 May 2021 amepitishwa na Baraza kuu la UVCCM kuwa Mwenyekiti mpya wa kamati ya Uchumi, Uwezeshaji na Fedha kupitia kikao cha Baraza Kuu ambacho kimemalizika jana Makao Makuu ya CCM Dodoma.

Kamati ya utekelezaji chini ya Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Komredi Kheri James ilikuja na pendekezo la jina la mwenyekiti huyo wa kamati ambapo baadae alithibitishwa na wajumbe kwa kura nyingi za ndio huku katibu wake akifahamika kwa jina la Rose Manumba, Baraza lilichagua wajumbe wengine wanne wa kamati kutoka bara na visiwani.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad