Gharama za wasanii kununua Views YouTube

 


Mtaalam wa masuala ya mitandao na mmiliki wa baadhi ya Akaunti za wasanii mitandaoni Mx Carter amefunguka mchezo wanaoufanya jinsi ya kununua 'views' feki kwenye mtandao wa YouTube.

 


Akizungumzia hilo kupitia EATV & EA Radio Digital Mx Carter amesema "Kuna website mbalimbali wanatengeneza robot ambao ni views feki ila YouTube wenyewe hawakubaliani na suala hilo na waliweka ugumu kiasi kwamba ukitaka kununua views gharama zake ni bei sana lakini kama unajiweza unaweza kununua".


"Athari za kununua views  YouTube kwa msanii huwa ni YouTube wenyewe kupitia video hizo za wasanii au channel zilizopo kwenye Platform yao na kushusha views feki, gharama zake ni kubwa japo wapo wanaofanya hivyo na wanapata pesa kupitia 'Digital platform' hizo" ameeleza Mx Carter


Taarifa hii imekuja baada ya Director Hanscana kuonesha jinsi wasanii wanavyonunua views YouTube jambo ambalo limezua gumzo mitandaoni

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad