Hali bado ni tete kati ya Israel na Palestina





Israel imeendelea kufanya mashambulizi ya angani huko Gaza huku wanamgambo wa Kipalestina wakiendelea kurusha maroketi kuyaelekeza upande wa Israel usiku wa kuamkia leo. 
Hakuna ishara ya mapigano hayo kuisha licha ya miito ya kimataifa ya kusitisha vita hivyo vilivyodumu kwa zaidi ya wiki moja sasa. 

Polisi ya Israel inasema wafanyakazi wawili raia wa Thailand wameuwawa na wengine saba kujeruhiwa baada ya shambulizi la roketi lililofanywa nje kidogo tu ya mpaka wa Gaza. 

Kundi la Hamas ambalo linatawala Ukanda wa Gaza na kundi la Islamic Jihad, yamekiri kuhusika na mashambulizi hayo. 

Jeshi la Israsel linasema karibu maroketi 50 yamerushwa kusini mwa mji wa Tel Aviv usiku kucha ila hakuna ripoti za majeruhi wala uharibifu wowote uliosababishwa na maroketi hayo. 

Msemaji wa jeshi la Israel amesema kwamba kundi la Hamas bado lina maroketi ya kutosha ya kufanya mashambulizi kwani hazina ya kundi hilo iliyoko Gaza bado ina maroketi karibu 12,000.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad