Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Mei 5, 2021 imefuta kesi ya kufanya mkusanyiko na kutotii amri halali katika geti la Gereza la Segerea iliyokuwa inawakabili watu 27 akiwemo Halima Mdee na wabunge wenzake wawili baada ya upande wa mashtaka kutopeleka mashahidi kwa ajili ya usikilizwaji wa shauri hilo.
Jumla ya watu 27 walikuwa wakikabiliwa na mashtaka matatu ambayo ni kukaidi amri, kufanya mkusanyiko usio halalu na kuharibu geti la gereza la Segerea, tukio walilodaiwa kulitenda Machi 13, 2020 katika eneo la Gereza la Segerea, Ilala jijini Dar es Salaam.
Wengine waliokuwa wakikabiliwa na kesi hiyo ni Ester Bulaya, Jesca Kishoa, aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob, Patrick Assenga na wengineo.