Mchezaji wa zamani wa Yanga na Simba Haruna Moshi amesema kuwa maandalizi ya mechi ya Dar es salaam Derby yanakuwa ya kipekee kutokana na utofauti wa ukubwa wa mtanange huo ambao unazikutanisha timu zenye mashabiki wengi nchini ambao ni watani wa jadi.
Akizungumza na EATV Boban amesema yoyote atayekuwa amejianda vizuri atashinda ila ni ngumu kutabiri yupi atashiinda kutokana na ugumu wa mechi hizo.
''Mandalizi ya Simba na Yanga yanakuwa ya kipekeake kutokana na mara nyingi viongozi wanakuja kambini kukaa na sisi kutupa maneno namna gani ambayo tutacheza na pia kutupa ahadi iwapo tutashinda".
Hata hivyo Nyota huyo wa zamani wa timu ya Taifa 'Taifa stars' Boban ijumaa ya wiki hii atahitimu mafunzo ya kozi ya FIFA ya Grassroots ambayo yanasimamiwa na mkufunzi kutoka katika shirikisho la mpira wa miguu nchini Raymond Gweba