Israel Wakubali Kusitisha Mapigano Dhidi ya Palestina




Wananchi wa Palestina wakishangilia baada ya Israel kukubali kusitisha mapigano.

MAELFU ya Wapalestina wamemiminika mitaani kushangilia makubaliano ya kusitisha mashambulizi kati ya Israel na wanamgambo wa Hamas, makubaliano hayo yaliyosimamiwa na Misri yalitangazwa usiku wa kuamkia leo Mei 21, Ijumaa.

 

Makubaliano ya kusitisha mashambulizi baina ya Israel na wanamgambo kutoka Palestina yameanza kutekelezwa usiku wa kuamkia Ijumaa.

 

Viongozi mbalimbali wamepongeza na kuyakaribisha makubaliano hayo ya kusitisha mashambulizi  kati ya makundi mawili ya wanamgambo wa Palestina Hamas na jingine linaloshikilia itikadi kali za Kiislamu.

 

Rais wa Marekani Joe Biden ameyakaribisha makubaliano hayo na ameeleza kuwa yanatoa nafasi muafaka kupiga hatua mbele baada ya siku 11 ya mashambulizi hatari, na kwamba amejitolea kwa hilo.

 

Punde tu muda wa kuanza utekelezaji wa makubaliano hayo ulipofika (saa nane usiku, majira ya Mashariki ya Kati), wakaazi wengi wa gaza walimiminika mitaani wakipaza sauti zao wakisema Mungu ni Mkubwa.

 

Ishara ya afueni baada ya mashambulizi makali yaliyowanyima nafasi ya kusherehekea Siku kuu ya Idd El-Fitr wiki iliyopita.

 M

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad