Jeshi la wanamaji la Marekani (USA) lilikamata meli yenye silaha iliyopatikana baada ya operesheni kaskazini mwa Bahari ya Arabia.
Kulingana na taarifa iliyotolewa na Kikosi cha 5 cha Jeshi la Wanamaji la Marekani, msafara w ameli ya makombora ulioongozwa na USS Monterey, ulikamata meli iliyosheheni silaha, kama sehemu ya operesheni iliyozinduliwa kaskazini mwa Bahari ya Arabia mnamo Mei 6.
Katika taarifa hiyo, iliripotiwa kuwa silaha hizo zilikuwa mikononi mwa Jeshi la Wanamaji la Marekani, lakini asili na usafirishaji wake bado unachunguzwa.
Ilielezwa kuwa baada ya kukamatwa, meli na wafanyakazi ambao mahojiano yao yalikamilishwa, waliruhusiwa kuondoka.
Inajulikana kuwa pande zinazohusika katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Yemen kwa miaka mingi zimesafirisha silaha kwenda nchini kupitia Bahari ya Arabia.
Nchi ya Yemen, ambayo imekuwa ikikumbwa na ukosefu wa utulivu wa kisiasa kwa muda mrefu, kuna mapigano kati ya Houthis inayoungwa mkono na Iran na vikosi vya serikali.
Wahouthi wameshikilia udhibiti wa mji mkuu wa Sana'a na baadhi ya mikoa tangu Septemba 2014, wakati vikosi vya muungano vinavyoongozwa na Saudi Arabia vimekuwa vikiunga mkono serikali ya Yemen dhidi ya Houthis tangu Machi 2015.