Jesse Lingard, mchezaji bora EPL

 

Winga wa West Ham United Jesse Lingard ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Aprili wa ligu kuu Egland, mchezaji huyo alifunga mabao manne na alipiga pasi moja ya usaidizi wa bao ndani ya mwezi huo.

Lingard anashinda tuzo hii baada ya kuikosa miezi mwili iliyopita mwezi Februari na Machi ambapo alishindwa kuitwaa tuzo hiyo. Hii ilikuwa ni mara ya tatu mfululizo Lingard anaingia kwenye kinyanganyiro cha kuwania tuzo ya mchezaji bora wa mwezi.

Winga huyu yupo West Ham kwa mkopo akitokea Manchester United, na ametwaa tuzo hii baada ya kuwashinda wachezaji Trent Alexander Arnold, Stuart Dallas, Mason Greenwood, Kelech Ihenacho, Matheus Pereira, Allan Saint Maximini na Chris Wood,alioingia nao fainali.

Na kocha Steve Bruce wa Newcatle United ameshinda tuzo ya kocha bora wa mwezi huo ikiwa ni kwa mara ya kwanza anashinda tuzo hiyo katika kipindi cha miaka 19. Bruce aliiongoza Newcastle kushinda michezo mwili na kutoka sare michezo miwili ndani ya mwezi Aprili kwenye michezo minne.

Steve Bruce ametwaa tuzo hiyo akiwashinda makocha Sam Allardyce, Marcelo Bielsa na Ole Gunnar Solskjaer

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad