Jumuiya ya kimataifa yaelezea wasiwasi juu ya ghasia za Jerusalem





Jumuiya ya kimataifa imeelezea wasiwasi mkubwa juu ya ghasia zinazoendelea mjini Jerusalem, siku moja baada ya makabiliano baina ya polisi wa Israel na Waplestina kujeruhi watu zaidi ya 200. 
Taarifa ya pamoja iliyotolewa na Marekani, Urusi, Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa, imeelezea kusikitishwa na kauli za uchochezi zilizotolewa na baadhi ya makundi ya kisiasa, pamoja na kurushwa kwa maroketi. 

Aidha taarifa hiyo pia imelaani kuanza tena urushaji maputo ya moto kutoka upande wa Gaza kuelekea Israel pamoja na kushambuliwa mashamba ya Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi. 

Licha ya kutolewa miito ya kimataifa, ghasia ziliendelea jana, huku watu wengi wakijeruhiwa wakati polisi wa Israel walipofyatua maji ya kuwasha na risasi za mipira kutawanya wandamanaji wa Kipalestina katika eneo la Jerusalem Mashariki.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad