Kaseke Aipeleka Yanga Nusu Fainali ASFC 2021

 


Mabingwa wa zamani wa kombe la Shirikisho nchini, klabu ya Yanga imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe hilo baada ya kuifunga timu ya Mwadui mabao 2-0 yaliyofungwa na kiungo wake Deus Kaseke kwenye dimba la CCM Kambarage mkoani Shinyanga.


Kaseke amefunga mabao hayo na kuendelea kuibeba Yanga kwenye mabega yake kwani ukiondoa mabao hayo mawili ya kuivusha timu, kaseka ana mabao 6 kwenye VPL, bao moja nyuma ya Yacouba Sogne mwenye mabao mengi, mabao 7 kwenye VPL.


Kaseka amezidi kuonesha kuwa yeye ni lulu kwenye kikosi hicho cha Wananchi kwa kufikisha bao lake la 9 msimu huu kwenye michuano yote ikiwa ni idadi yake ya mabao mengi zaidi kwenye msimu mmoja akiwa na Yanga.


Ushindi huo unaifanya Yanga kukutana na klabu ya Biashara United Mara kwenye hatua ya Nusu fainali ya michuano hiyo huku Mwadui amehitimisha msimu wake kwa kushuka daraja kutoka Ligi kuu Bara na kwenda ligi daraja la kwanza.


Yanga imepata ushindi huo licha ya kuwakosa nyota wake kadhaa kutokana na sababu mbalimbali, mshambuliaji Michael Sarpong, mlinzi wa kati Lamine Moro, mlinda mlango Metacha Mnata wakikosekana kutokana na sababu za utovu wa nidhamu.


Kiungo mkongwe, Haruna Niyonzima amekosekana kutokana na sababu za kifamilia huku viungo washambuliaji Said Ntibazonkiza, Carlinhos na mlinzi Yassin Mustapha wakiwa na majeraha.


Michezo ya michuano hiyo itakayoendelea kesho, ni ule utakaowakutanisha Rhino Rangers dhidi ya Azam saa 10:00 jioni kwenye dimba la CCM Kambarage ilhali Bingwa mtetezi klabu ya Simba itajitupa kwenye dimba la Mkapa jijini Dar es Salaam kukipiga na Dodoma Jiji saa 1:00 usiku

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad