Kenya yaondoa marufuku ya watu kutoka nje ‘Lockdown’




Katika kusheherekea siku ya wafanyakazi duniani, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametangaza kuondoa zuio la watu kutotoka nje katika kaunti tano nchini humo kwa ajili ya kukabiliana na virusi vya corona.



Katika taarifa yake rais Kenyatta amesema wakati alipotoa agizo la pili kwa umma mnamo Machi 2021, la jinsi ya kukabiliana na janga la Corona, Nairobi ilikuwa na maambukizi 56,815.

Maambukizi yalipungua mwezi Aprili kwa chini ya 15,000, hii ikionesha asilimia 74% ya maambukizi yamepungua mjini Nairobi.

 Takwimu za wataalamu wetu wa afya zinaonesha hali kama hiyo katika eneo ambalo tuliweka katazo la watu kutotoka nje mwezi Machi 26, 2021.

Baada ya mwezi mmoja wa marufuku ya kutoka nje , kesi za maambukizi ya COVID yamepungua mpaka 72%.

Maeneo mengine ya nchi , maambukizi ya COVID yamepungua kwa 89% Mombasa na 90% Busia kati ya mwezi Machi na Aprili 2021.

KENYA
 Kufuatana na ushahidi wa wataalamu, na baraza la usalama la Taifa pamoja na tume kitengo cha dharura cha janga la Covid-19, leo hii uamuzi ufuatao umefikiwa;

Maeneo ambayo yalikuwa na marufuku ya kutoka nje ya maeneo Nairobi, Machakos, Kiambu, Kajiado na Nakuru, zuio hilo limeondolewa.
Saa za marufuku ya kutoka nje yanaanza saa nne usiku mpaka saa kumi alfajiri, inaanza kuanzia leo Mei Mosi 2021 katika nchi nzima , mpaka taarifa zaidi itakapotolewa. Awali marufuku hiyo ilianza saa mbili usiku hadi saa kumi alfajiri katika kaunti tano zilizowekewa marufuku ya kutoka nje ilhali maeneo mengine za taifa hilo ilianza saa nne usiku hadi saa kumi alfajiri.
Mikusanyiko ya kidini itarudi ikiwa inazingatia muongozo wa wizara ya afya. Hata hivyo nyumba ya ibada inapaswa kuwa na watu theluthi katika jengo la kuabudia .
Huduma za migahawa na maeneo mengine ya chakula yatarudi kuendelea na kazi kwa kuzingatia muongozo wa wizara ya afya pamoja na wizara ya utalii. Wenye migahawa wanashauriwa kutumia maeneo ya nje ili kuepuka mkusanyiko na watu waweze kuachiana nafasi.
Shule zimefunguliwa na kutakiwa kufuata miogozo ya afya katika kukabiliana na janga la corona.
Shughuli za michezo zimefunguliwa
Mihadhara ya kisiasa bado imekatazwa
Waajiri wamesisitizwa kuwaachia wafanyakazi wafanye kazi nyumbani
Masharti yaliyowekwa kwenye zuio la siku 30 Kenya

kenya
Kufuatia ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona kenya ilifungia kaunti tano kutotoka nje, ambazo ni Kajiado, Machakos, Kiambu na Nakuru .

Kulikuwa hakuna usafiri wa barabarani ,angani na reli utakaoruhusiwa kuingia na kutoka sehemu hizo zilizotajwa kuathiriwa sana na Corona’.

Maeneo hayo yalitakiwa kuwa chini ya masharti hayo ya zuio kwa siku 30 kwa kuwa rais Kenyatta alisema kiwango cha maambukizi kilizidi mara kumi zaidi.

Kando na kuzuia usafiri wa watu katika kaunti hizo tano rais Kenyatta pia alipiga marufuku mikutano au mikusanyko ya watu katika maeneo hayo.

Ingawa safari za usafiri wa kigeni ziliendelea kwa kufuata masharti dhidi ya kukabiliana na corona.

Shughuli zote za kuabudu katika kaunti za Nairobi, Nakuru, Machakos, Kiambu, na Kajiado zilizuiwa hadi wakati uamuzi huo utakapobadilishwa .

Masomo ya ana kwa ana yaliondolewa na vyuo vikuu vyote na shule kufungwa .

Wafanyakazi wa mashirika ya serikali na ya kibinafsi walitakiwa kufanyia kazi nyumbani isipokuwa kwa wale wanaotekeleza uduma muhimu zinazowahiaji kwenda kazini.

Mikutano yote itakayoruhusiwa itakuwa na watu wasiozidi 50 ilhali mazishi yataandaliwa ndani ya kipindi cha saa 72 na ni watu 50 pekee watakaoruhisiwa mazishini .


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad