Kocha Simba: Tunatakiwa Kushinda Mbele Ya Yanga





KUELEKEA kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba dhidi ya Yanga, kesho Mei 8, 2021 uongozi wa Simba umeweka wazi kwamba unatakiwa kushinda mchezo huo ili kuongeza nafasi ya kushinda taji la ligi.

Simba ni mabingwa watetezi wa ligi kesho wanakutana na Yanga kwenye mchezo wa ligi unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Walipokutana mzunguko wa kwanza Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Yanga 1-1 Simba na watupiaji kwa Yanga alikuwa ni Michael Sarpong na kwa Simba alikuwa ni Joash Onyango ilikuwa ni Novemba 7,2020.

Seleman Matola, Kocha Msaidizi wa Simba amesema kuwa wana kazi moja ya kufanya kesho kusaka ushindi ili kuongeza nafasi ya kuweza kutetea taji hilo.

“Utakuwa ni mchezo mgumu na wenye ushindani ila lazima tushinde ili tuweze kuongeza nafasi ya kutetea taji letu la ligi.

“Mbali na kucheza pia ni muhimu tufanye kazi ya umiliki wa mpira kama ambavyo tumekuwa tukifanya kwenye mechi zetu ambazo zimepita ili kuwapa burudani mashabiki hivyo wajitokeze kutupa sapoti hatutawaangusha,”.

 

“Inabidi tushinde mchezo wa kesho ili tuwe na nafasi nzuri ya kutetea ubingwa. Tunataka tukawape watu burudani, lazima tukacheze mchezo ambao tumezoea kucheza na siku zote timu inayomiliki mpira ina nafasi kubwa ya kupata matokeo. Tunawambia mashabiki wetu waje kutushangilia, hatutawaangu amesema Matola

Kwenye msimamo Simba ipo nafasi ya kwanza baada ya kucheza mechi 25 ina pointi 61, Yanga ipo nafasi ya pili ina pointi 57 baada ya kucheza mechi 27.

 


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad