Korea Kaskazini Yakataa Mazungumzo na Marekani





KOREA Kaskazini imepuuza wazo la kufanya mazungumzo na Marekani siku moja baa ya serikali ya Rais Joe Biden kusema uko tayari kwa majadiliano ya kidiplomasia kuhusu Pyongyang kuachana na mradi wake wa nyuklia.

 

Wizara ya mambo ya kigeni ya Korea Kaskazini imesema haiko tayari kufanya mazungumzo na taifa linalotumia diplomasia “bandia” kuficha matendo yake ya uchokozi.

 

Taifa hilo pia limemtahadharisha rais Joe Biden wa Marekani dhidi ya kuchukua kile imekitaja kuwa “msimamo uliopitwa na wakati” na kuonya kuwa Washington itapata madhara kwa kuichokoza Korea Kaskazini.

 

Matamshi kutoka Pyongyang yanatolewa siku kadhaa tangu rais Biden alipoliambia bunge la Marekani kuwa utawala wake utatumia diplomasia pamoja na msimamo usioyumba kudhibiti malengo ya nyuklia ya Korea.

 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad