KUELEKEA kwenye mchezo wa Dabi ya Kariakoo, kesho Jumamosi, inadaiwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Mohamed Dewji ‘Mo’, anatarajiwa kuzungumza na wachezaji pamoja na benchi la ufundi kwa njia ya simu, akiwa Abu Dhabi.
Mo ameshatoa taarifa hiyo kwa uongozi wa Simba, ambapo atatumia muda huo kutoa hamasa kwa wachezaji, kuelekea kwenye mechi hiyo ya kesho.
Taarifa za ndani ya klabu zinaeleza kuwa ratiba hiyo ya kupiga simu ilikuwa iwe jana Alhamisi au leo Ijumaa.
Baadhi ya baadhi ya vigogo wa Simba waliongozwa na Mtendaji Mkuu (CEO) wao, Barbara Gonzalez kwenda kambini kuzungumza na wachezaji ambapo waliahidi mambo mbalimbali endapo watafanikiwa kuifunga Yanga.
“Kweli wachezaji walizungumza na baadhi ya viongozi wetu na kubwa lilikuwa ni kuongeza hamasa, na wao kuonyesha nia yao ya dhati katika ushiriki wao kuelekea mechi yetu ya Jumamosi dhidi ya Yanga, kwa ufupi tu naomba nikujuze kwamba, ratiba iliyopo sasa tunasubiria kuzungumza na Mo ambaye yupo nje ya nchi.
“Tayari maandalizi yote juu ya hilo yameshafanyika, hivyo kila mmoja ana taarifa ambapo kama hakutakuwa na mabadiliko yawezekana usiku wa leo (jana Alhamisi) au kesho (leo Ijumaa), tutaongea naye kwa njia ya mtandao na tuna mtumaini makubwa na kikao chake hicho ambapo tunaamini kwa namna yoyote atatangaza dau nono,” kilisema chanzo