Kuna tatizo kwenye kununua LUKU- TANESCO



Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeomba radhi wateja wake kutokana na hitilafu iliyotokea kwenye Mfumo wa Manunuzi ya Umeme wa LUKU.
Hitilafu hiyo imetokea kuanzia Mei 17, 2021 na kusababisha baadhi ya wateja kushindwa kununua umeme.

TANESCO imeomba uvumilivu kwa muda huu ambao tatizo linaendelea kutatuliwa.

“Tunawaomba radhi kutokana na hitilafu iliyotokea kwenye mfumo wa manunuzi ya umeme wa LUKU siku ya Jumatatu, Mei 17, 2021 na kusababisha baadhi ya wateja kushindwa kununua umeme. Tunaomba uvumilivu wakati wataalamu wetu wanafanya kazi kuhakikisha tatizo hilo linatatuliwa haraka” TANESCO 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad