Kwanini Waandishi na Wachambuzi wa Michezo wanamuogopa Haji Manara?



Hivi karibuni waandishi na wachambuzi wa soka wamekuwa wakimuogopa sana Haji Manara jambo ambalo nilikuwa naliona kwa mbali sana lakini kwa sasa limekuwa kubwa sana kiasi kwamba wachambuzi hawawezi tena kusema kwa uwazi madhaifu ya simba bila kupamba pamba na kupongeza kwanza kuogopa kukabiliwa vikali au kugombana na Haji Manara.


Nilishangazwa zaidi alipo waita taka taka waliogopa kukemea lakini bali ni wachache ndio walikuwa wana uwezo huo wachambuzi kama kina Shafii,Maulid Kitenge,Jemedari Saidi na Oscar Oscar ndio huwa hawamuogopi kumsema.


Yani nimeshangazwa sana zaidi wiki hii baada ya simba kutolewa hakuna anayethubutu kusema simba katolewa bali kila mmoja anatafuta kaurembo kake ... oohh kafa kiume,wamepambana, wamepigana, wengine wanasema hawajatolewa kifala ... hii yote ni kumuogopa Manara? maana ana uwezo wa kuzuia wasitangaze maudhui ya simba? Kwanini wachambuzi wanaogopa kusema simba amefungwa na kutolewa kwa uzembe wake?


Kwanini wanamuogopa sana Haji Manara?

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad