Msanii Nuh Mziwanda amekiri ule msemo unaosema "ustaa ni mzigo wa mwiba ukiubeba unaumia" baada ya kutuhumiwa kuchukua pesa za watu na kusepa nazo ambazo alitakiwa akafanye show sikukuu ya Eid.
Taarifa hiyo imetolewa na mmiliki mmoja wa Lounge ambaye anasema walikubaliana kila kitu na Nuh Mziwanda ambapo alianza kumtumia 'Advance' ya Tsh Laki Moja.
Sasa kupitia EATV & EA Radio Digital Nuh Mziwanda ametolea maelezo taarifa hiyo kwa kusema "Nimepata hayo malalamiko, ustaa ni mzigo wa mwiba ukiubeba unaumia hata Fid Q alisema, hivyo ni vitu vya kawaida na vinatokea sana kwenye maisha yetu kitu ila kilichoni-cost kwenye hilo jambo ni mimi kuweza kusaidia kwa sababu nilikuwa natoa msaada".
"Jamaa alinipigia simu akasema ana-party siku ya Eid hivyo akaniomba niende kama 'Special appearance' nikamwambia nikipata show sitakuja ila nisipopata nakuja, tukakubaliana bei ya special appearance ili nioneakane tu na wala sio show"
"Wakanitumia advance ya Laki moja,mida ya saa 9 Mchana watu wa Kigali wakanitumia tiketi nikafanye Show Rwanda na nikampa taarifa kwamba tutafanya siku nyingine au niwarudishie pesa yao, mara jamaa akaanza kunitumia message za vitisho kwamba tutakutana BASATA, Mahakamani au Redioni" ameeleza Nuh.