Mahakama Kuu ya Tanzania yatupilia mbali wosia wa Dkt. Mengi





Jaji Mlyambina wa Mahakama Kuu ya Tanzania amesema wosia wa Marehemu Dkt. Reginald Mengi ulioandikwa Agosti 17, 2017 haukuzingatia misingi ya kisheria ya uandishi wa wosia
Mahakama imesema, wosia huo ulibagua na kutowaweka katika mirathi baadhi ya watoto bila sababu huku ukiwabakisha Jacqueline Ntuyabaliwe-Mengi na watoto mapacha kuwa ndio warithi

Pia, wosia huu unaonesha kuwa, Marehemu Dkt. Reginald Mengi amegawa mali nyingine ambazo si zake pekee yake

Mahakama imesema kuwa, wosia huo uliandikwa kipindi ambacho Marehemu Mengi alikuwa hana uwezo wa kuandika wosia kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimsumbua tokea mwaka 2016

Aidha, Mahakama Kuu ya Tanzania imewachagua Abdiel Mengi na Benjamin Mengi kuwa Wasimamizi wa Mirathi ya mali alizoacha Dkt. Mengi. Maamuzi haya yameagiza mgawanyo wa mali uanze mara moja

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad