Aliyekuwa Mgombea wa Ubunge Jimbo la Bukoba Mjini kupitia CHADEMA, Chief Kalumuna pamoja na wenzake waliokuwa wanakabiliwa na tuhuma 8 wameachiwa huru na Mahakama ya Bukoba.
Kalumuna amesema Mgombea Ubunge, Madiwani pamoja na Mawakala walitakiwa kula kiapo siku 7 kabla ya Uchaguzi lakini walipokwenda kufanya hivyo Mkurugenzi alikataa ili wasiwe na sifa ya kwenda kuhesabu Kura.
Amefafanua, “Alipokataa ikizuka taharuki kubwa katika Viwanja vya Kaitaba, mimi na wafuasi wangu wakatukamata wakatuweka ndani, watakufungulia Mashtaka yenye ‘charges’ 8”. Amesema Serikali iliwashtaki kwa kufanya fujo na vurugu kipindi cha Uchaguzi.