Mamlaka za afya nchini Malawi zinatarajiwa kuharibu zaidi ya dozi 19,000 za chanjo ya Covid 19 kutoka AstraZeneca baadaye siku ya Jumatano.
Wanasema chanjo hizo zimepitisha muda wa matumizi na hakuna data ya kutosha kujua ikiwa ni salama kutumiwa, kufuatia mwongozo kutoka kwa Shirika la Afya Duniani ,WHO .
Itakuwa nchi ya kwanza ya Kiafrika kuharibu hadharani chanjo zilizopitisha muda wa matumizi .
Mamlaka zinasema hatua hiyo inataka kuwapa imani Wamalawi kupata chanjo dhidi ya Corona wakati inapopatikana.
Kufikia sasa, ni watu wachahe waliopewa yaCovid-19 nchini humo , haswa kwa sababu ya habari potofu iliyoenea juu ya matumizi yake.
Maafisa wanaogopa kwamba kutumia chanjo iliyopita tarehe ya kutumiwa itawaogofya raia kukubali kuchanjwa .
Walakini serikali nchini Malawi ina matumaini kuwa idadi ya watakaokubali kuchanjwa itaongezeka mara tu watakapopata shehena ifuatayo kutokaCovax.
Zaidi ya Wamalawi 330,000 wamepewa chanjo hiyo